Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Matukio hayo yalifanyika jana, tarehe 25 Juni 2026, ambapo matembezi ya amani yaliandaliwa na JAMAT Khoja na kuhusisha ushiriki wa waumini wengi waliotembea kwa utulivu na nidhamu wakibeba ujumbe wa amani, haki na kupinga dhuluma.
Mbali na matembezi hayo, waumini walishiriki pia katika vikao vya maombolezo (Majlis) vilivyoangazia malengo ya harakati za Imam Hussein (as), mafunzo ya tukio la Karbala, na umuhimu wa kuendeleza maadili ya uadilifu, kujitolea na kusimama dhidi ya dhuluma.
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |








Maoni yako